Wakurugenzi wawili wa polisi wauawa Iraq
3 Aprili 2004Matangazo
BAGHDAD: Nchini Iraq watu wasiojulikana wamempiga risasi na kumwua mkurugenzi wa polisi wa Al Mahmudiyyah, ulio mtaa wa mji mkuu Baghdad, liliarifu Shirika la Utangazaji la Kiarabu Al Jazeera. Pia hapo jana aliuawa katika gari yake mkuu wa polisi wa mji wa Kufa ulio Kusini mwa mji mkuu. Pia Al Jazeera limeripoti kuuawa kwa wakazi wawili wa nyumba iliyoshambuliwa kwa kombora. Na wanajeshi wa Kispania wamemtia nguvuni mwendesha afisi wa Kishiya mwenye itikadi kali Moktada Sadr ambaye ni mojawapo wa wapinzani wakubwa wa uvamizi wa Wamarekani nchini Iraq. Na watu walioshuhudia wameripoti kuwa Waarabu na Waturkmenia wapatao 1000 wamefanya maandamano mjini Kirkuk huko Iraq ya Kaskazini kupinga madaraka makubwa waliodhibiti Wakurdi mjini humo.