MigogoroUrusi
Uswisi yawaghadhabisha wakosoaji wa Kremlin
31 Julai 2025Matangazo
Wakosoaji hao ni pamoja na wafungwa wa zamani wa kisiasa.
Barua ya wazi iliyotiwa saini na wafungwa wa zamani wa kisiasa Vladimir Kara-Murza, Oleg Orlov na Ilya Yashin, miongoni mwa wengine, iliishutumu Uswisi kwa kuwa mwenyeji wa washirika wakuu wa Putin, huku Urusi ikiendelea na vita dhidi ya Ukraine.
Ujumbe huo wa Kremlin unaoongozwa na Spika wa Bunge Valentina Matvienko, uliwasili Geneva siku ya Jumapili kushiriki mkutano wa siku tatu wa wabunge wa kimataifa.
Hii ni ziara ya ngazi ya juu zaidi kutoka Urusi, barani Ulaya tangu taifa hilo lilipoivamia Ukraine. Wapinzani wa Rais Vladimir Putin wanahofia kwamba baadhi ya madola na taasisi za magharibi huenda zikarekebisha uhusiano na Moscow licha ya uvamizi wake.