MigogoroAfrika
Uhaba wa chakula wawaondoa wakimbizi 6,000 Kenya
29 Agosti 2025Matangazo
Taarifa ya Umoja wa Mataifa iliyotoa takwimu hizo hata hivyo imesema idadi kamili ya wakimbizi walioondoka kambini huenda ni kubwa zaidi kwa kuwa wengi wao hutumia njia zisizo rasmi kuondoka. Imeongeza kuwa kama fedha zaidi zisipotolewa kwa ajili ya wakimbizi, wengi wao watalazimika kukabiliana na njaa ndani ya kambi au kurejea nyumbani ambako hali bado ni tete. Itakumbukwa kuwa kambi ya Kakuma iliyo kaskazini mwa Kenya inawahifadhi wakimbizi karibu laki tatu kutoka Sudan Kusini, Somalia, Uganda na Burundi.