Wakimbizi wa Syria wameanza kurejea kwao kutoka Ujerumani
7 Septemba 2025Matangazo
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ujerumani imesema kufikia Agosti, Wasyria 1,867 walirudi nyumbani kwa msaada wa serikali, huku wengine wakiondoka kupitia programu za majimbo au bila msaada.
Kwa sasa zaidi ya wa Syria 955,000 wanaendelea kuishi Ujerumani, ambapo mwaka jana pekee 83,000 walipata uraia na maombi mapya ya hifadhi 17,650 yaliwasilishwa.
Serikali imesisitiza kuwa inajitahidi kuwezesha kurejea kwa hiari, lakini hakuna urejeshaji wa lazima uliofanyika tangu 2012, tofauti na Austria ambayo tayari imerudisha mtu mmoja.