Wakenya waliokwama Myanmar warejea nchini
7 Aprili 2025Idadi hiyo inafikisha mpaka sasa, raia wa Kenya mia moja na hamsini na tatu- 153, ambao wameokolewa kutoka mikononi mwa walaghai nchini Mynamar.
Kwa mujibu wa waathiriwa kadhaa, safari yao ilianzia hapa nchini Kenya walipoahidiwa kazi zenye malipo mazuri nchini Thailand na mawakala wa hapa Kenya.
Wakiwa na matumaini makubwa, walijitahidi kupata hati muhimu za kusafiria pamoja na fedha za gharama za safari, bila kujua kuwa walikuwa wakielekea kwenye jinamizi. Jamaa huyu aliyejifunika kwa barakoa anajitambulisha kwa jina Dan, anaelezea kadhia yake.
"Ilikuwa tuibie watu on-line, umchanganye mtu na uibe, hakuna serikali huko, huko unafanyiwa kitu chochote.
Wakati wa kuwapokea waliorejea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Katibu Mkuu wa Masuala ya Diaspora, Roseline Njogu, aMasaibu ya kusaka ajira ughaibuni, baadhi ya Wakenya wakwama Myanmarliwaonya Wakenya dhidi ya kushirikiana na mawakala au kampuni za utalii ambazo hazijasajiliwa kisheria.
Soma pia:Dhuluma za kimapenzi, ulanguzi wa binadamu na nyinginezo zaongezeka Busia
Serikali imesisitiza kuwa kwa sasa hakuna nafasi za kazi kwa Wakenya katika eneo la ‘Golden Triangle' huko Kusini Mashariki mwa Asia.
Imeongeza kuwa wakala au kampuni yoyote inayodai kuwa na ajira katika eneo hilo inapaswa kuchukuliwa kuwa ni walanguzi wa binadamuna iripotiwe mara moja kwa Idara ya Masuala ya Diaspora au kituo cha polisi kilicho karibu.
"Kila mtu husema anaenda Thailand, ilhali wanakwenda Mynmar, na wanakwenda kule kama watalii, hivyo inakuwa vigumu kuwafutailia kama wizara sababu wanasafiri na viza ya watalii.
Ulaghai ndani ya safari yao ya kikazi
Waathiriwa wengi walieleza kuwa walipowasili, walipatwa na mshangao mkubwa walipogundua kuwa hawakuwa wamewasili Thailand, bali Myanmar.
Waathiriwa walielezea hali waliyoikuta Myanmar kama ya kutisha. Wengi walifungiwa ndani ya jengo lililojaa kompyuta na kulazimishwa kushiriki katika ulaghai wa mitandaoni.
"Nataka kurudia hakuna kazi Thailand, ukipata kazi ya kuosha choo, hata kama unalipwa shilingi 50 heri hapo kuliko Thailand.” Alisema mmoja wa waathirika ambaye alitaka jina leke lihifadhiwe
"Mimi nilikuwa nafanya kazi Nairobi, lakini nilipata ofa ya kusafiri Thailand kumbe uwongo." Mwathirika mwingine aliiambia DW namna alivyoacha kazi yake na kutumbukia kwenye ulaghai wa ajira nje ya Kenya.
Soma pia:Mpango wa AGOA na hatma ya mamia ya ajira Kenya
Baadhi walishuhudia wenzao wakifariki kutokana na mateso hayo. Walifichua kuwa walifungiwa ndani ya chumba kikubwa kilichojaa kompyuta na kulazimishwa kuwadanganya watu mitandaoni.
Wale waliokosa kufikia malengo waliwekwa kwenye vyumba vya giza na kuteswa. Wakenya hao mia moja na hamsini na tatu, 153, walikuwa miongoni mwa watu zaidi ya 7000 wa mataifa mbalimbali waliookolewa kutoka kwenye kambi hizo za udanganyifu baada ya oparesheni ya uokoaji ya kimataifa ikishirikiana na Serikali ya Ufalme wa Thailand.