JangaAfrika
Wakenya 2 wafungwa miaka 30 kwa kula njama na magaidi
20 Juni 2025Matangazo
Shambulizi hilo liliilenga hoteli moja ya fahari kwenye mji mkuu Nairobi na kusababisha vifo vya watu 21.
Mahakama ilipatiwa ushahidi uloonesha kuwa Hussein Mohammed Abdille Ali na Mohammed Abdi Ali, wote raia wa Kenya, waliwasaidia wanamgambo wa itikadi kali kupata vitambulisho bandia vilivyowawezesha kuishambulia hoteli ya DusitD2.
Kundi la itikadi kali la Al Shaabab linaloendesha shughuli zake kwenye taifa jirani la Somalia, lilidai kuhusika na shambulio hilo la kutisha ndani ya Kenya.
Shambulizi hilo lilitokea miaka 6 tangu watu 67 walipouawa kwenye shambulizi lililolilenga duka kubwa la Westgate na miaka minne baada ya wanamgambo kuwaua watu 147 walipokishambulia Chuo Kikuu cha Garissa kaskazini mwa Kenya.