Kama ilivyo katika maeneo mengine duniani Wakristo Wakatoliki nchini Tanzania, wanaomboleza kifo cha kiongozi wa kanisa hilo Papa Francis kilichotokea Jumatatu ya Aprili 21. Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania TEC, limesema Watanzania wanaotaka kutoa salamu za rambirambi kwa Kanisa Katoliki, wanatakiwa kwenda ubalozi wa Papa jijini Dar es Salaam. Sikiliza ripoti ya Veronica Natalis.