Taka imekuwa ni kero kubwa na kuhatarisha afya ya jamii katika moja ya kitongoji katika mji wa kiuchumi Ivory Coast Abidjan, kundi la vijana limeamua kutosubiri mamlaka kuchukua hatua, wameamua kutengeneza mifumo ya maji taka ili kuondoa tatizo kadhalika kuleta ustawi wa afya ya jamii katika eneo husika.