Wajumbe wa Urusi na Ukraine wakutana Istanbul
2 Juni 2025Matangazo
Wajumbe kutoka Urusi na Ukraine wamekutana nchini Uturuki leo Jumatatu,kushiriki duru ya pili ya mazungumzo ya moja kwa moja ya kujaribu kutafuta makubaliano ya kumaliza vita nchini Ukraine.
Mazungumzo hayo yanafanyika zaidi ya wiki mbili baada ya duru ya kwanza, huku kukiwa hakuna matumaini makubwa ya kupigwa hatua.
Ujumbe waUkraineunaongozwa na waziri wa ulinzi wa nchi hiyo Rustem Umerov huku Urusi ikiongozwa na msaidizi wa rais Vladmir Putin, Vladmir Medinsky.
Maafisa wa Uturuki wamefahamisha kwamba mkutano huo utakaoshirikisha pia shirika la ujasusi la Uturuki, utaongozwa na waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Hakan Fidan kuanzia saa saba kwa saa za Uturuki.