Wajumbe wa amani wa Urusi na Ukraine kukutana Saudia
22 Machi 2025Kiongozi wa ujumbe wa Urusi kwenye mazungumzo ya kusaka amani na Ukraine, Grigory Karasin, amesema serikali mjini Moscow inatumai kwamba mazungumzo ya kusitisha mapigano kati Urusi na Ukraine yatakayofanyika siku ya Jumatatu nchini Saudia Arabia yatafanikiwa.
Mazungumzo hayo yanatarajiwa kufanyika siku chache baada ya Urusi kukataa pendekezo la Marekani na Ukraine la kusitisha mapigano kwa siku 30 na badala yake ikapendekeza ushitishwaji mashambulizi ya anga dhidi ya miundombinu ya nishati.
Soma zaidi.Israel na Lebanon zaingia kwenye mvutano mpya wa kiusalama
Marekani ambayo ndio mpatanishi itafanya mazungumzo ya wakati mmoja na wajumbe wa Ukraine na Urusi katika katika jitihada za kufanikisha usitishaji wa vita vinavyoendelea kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.
Huko katika uwanja wa vita nchi hizo zimeripoti hii leo mashambulizi kutoka pande zote mbili.