Wajerumani wawili wauawa Iraq:
16 Machi 2004Matangazo
BAGHDAD: Wajerumani wawili wameuawa katika shambulio huko Iraq, kwa kulingana na taarifa zilizowafikiana za polisi wa Iraq na msemaji wa wanajeshi wa Kimarekani. Kwa mujibu wa habari hiyo inayothibitisha taarifa ya mauwaji hayo iliyotangazwa mapema na Shirika la Televisheni ya Ujerumani, ZDF, gari ya wahandisi hao wawili wa Kijerumani ilishambuliwa na watu wasiojulikana karibu ya mji wa Mussayab, KM kama 70 Kusini mwa mji mkuu Baghdad. Katika shambulio hilo waliuawa pia polisi wawili wa Kiiraq.