Waisrael waandamana kuunga mkono mateka walioko Gaza
17 Agosti 2025Matangazo
Hatua hiyo inafanyika ikiwa ni takriban miaka miwili baada ya kutekwa kwao. Waandamanaji walifunga barabara kote nchini Israel, ikiwemo barabara kuu mjini Tel Aviv, wakipeperusha bendera za Israeli za rangi ya bluu na nyeupe pamoja na bendera za manjano zinazowakilisha mshikamano na mateka.Waandamanaji wanaitaka serikali kumaliza mara moja vita vya Gaza, kufanikisha makubaliano ya kuwaachilia mateka, na kubatilisha uamuzi wake wa hivi karibuni wa kupanua operesheni za kijeshi katika Jiji la Gaza.Muunganiko wa familia za mateka na ndugu wa jamaa ambao hawajulikani walipo hadi wakati huu, ulitoa wito wa kufanyika mgomo wa kitaifa leo hii kwa shabaha ya hatua hiyo iendane na mwanzo wa juma la kazi nchini humo.