Waislamu nchini Tanzania wamesheherekea sikukuu ya Eid ul Fitr leo Jumatatu baada ya kundi lengine kusheherekea jana. Katika msikiti wa Mohamed wa Tano uliopo katika makao makuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania BAKWATA Kinondoni jijini Dar es Salaam, waumini wameungana na Rais Samia Suluhu Hassan kutimiza ibada hio muhimu inayohitimisha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.