Kuna nchi chache ambapo baadhi ya mitandao ya kijamii imepigwa marufuku ama kuzuiwa kabisa. Mojawapo ya nchi hizo ni Iran. Katika makala ya Sema Uvume, Elizabeth Shoo anakufahamisha kwanini mitandao hiyo imefungwa, wananchi wanafanyaje kukiuka marufuku hiyo na pia anazungumza na mwanamke wa Kiiran anayeendesha kampeni mtandaoni kupinga masharti ya kuvaa hijabu.