MigogoroYemen
Wahuthi wanuia kuanza tena kushambulia meli za Israel
12 Machi 2025Matangazo
Waasi hao wa Huthi wamesema watazipiga marufuku meli zote za Israeli kupita kwenye Bahari ya Shamu, Bahari ya Arabia, Mlango wa Bahari wa Baba al-Mandab na Ghuba ya Aden baada ya kushindwa kutimiza masharti yaliyowekwa na waasi hao Ijumaa iliyopita.
Israel ilizuia misaada yote katika Ukanda wa Gaza ulioharibiwa na vita zaidi ya wiki moja iliyopita, ikiishinikiza Hamas kuwaachilia mateka waliosalia.
Waasi hao wamesema marufuku hiyo itaanza kutekelezwa baada ya tangazo hilo na kuongeza kuwa mashambulizi yataendelea hadi Israel itakaporuhusu kupelekwa misaada huko Gaza.