Wahouthi wafyetua kombora lilolenga Kaskazini mwa Israel
23 Aprili 2025Waasi wa Houthi nchini Yemen wamefyetuwa kombora kuelekea Kaskazini mwa Israel leo Jumatano, na kusababisha ving'ora kusikika katika miji ya Haifa, Krayot na maeneo mengine magharibi mwa bahari ya Galilee.Soma pia: Mashambulizi ya Marekani nchini Yemen yaua watu 74
Jeshi la Israel limesema mifumo yake ya ulinzi ilifanikiwa kwa kiasi fulani kuzuia kombora hilo. Hata hivyo, kundi hilo la waasi, halikuthibitisha mara moja kufanya shambulizi hilo, japo inaweza kuchukuwa saa kadhaa au hata siku kadhaa kabla ya kujitokeza kuthibitisha.Soma pia:Waasi wa Huothi washambulia kwa kombora Israel
Kwa upande mwingine lakini kundi hilo kupitia msemaji wake, Brigedia Jenerali Yahya Saree limedai kudunguwa droni nyingine ya mashambulizi aina ya MQ-9 iliyorushwa katika anga ya Yemen.
Jeshi la Marekani limekiri kuhusu ripoti ya kudunguliwa droni hiyo ingawa haikuwa tayari kutowa maelezo zaidi.