Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wachambua
30 Juni 2005Tuanzie na siasa ya ndani ya Ujerumani.Kesho kansela Gerhard Schröder atawataka wabunge watamke kama wana imani nae au la.Imepangwa tangu mwanzo lakini kura hiyo ya imani ishindwe,ili uchaguzi upate kuitishwa mwaka mmoja kabla ya wakati.Gazeti la FRANKFURTER ALLGEMEINE ZEITUNG linaandika:
„“Eti eti hazishi,watu wanaendelea kujiuliza, eti vipi kansela Gerhard Schröder ataweza kuwatanabahisha washirika katika serikali yake ya muungano,na ambao ndio wanaodhibiti wingi wa viti katika bunge la shirikisho Bundestag,wasimpe imani yao, bila ya mwenyewe kuonekana kama hafai kutetea tena wadhifa huo?Baada ya hoja ambazo yeye na Münterfering wamekua wakizitoa siku hadi siku,itamuia vigumu sasa kuzusha maajabu mengine.Serikali kuu ya Ujerumani,chini ya muundo wake wa sasa muda wake unaonyesha umeshamalizika.Shröder lakini anabidi amtanabahishe zaidi rais wa shirikisho juu ya hali hiyo.
Gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG linaandika:
„Ripoti,eti Schröder alikejeli mbele ya mawaziri wake,akisema wakosoaji wake wakubwa sasa wanamuunga mkono,hazijakanushwa mpaka sasa.Kura ya imani kwa namna hiyo imeshajibiwa-japo kwa namna nyengine.Schröder anawatilia shaka wabunge wa chama chake,kinyume na jinsi sheria msingi inavyoeleza.“
Hata gazeti la MANNHEIMER MORGEN linaukosoa uamuzi wa kansela.Gazeti linaandika:
„ Kama Schröder anahisi amefungika, kwanini basi hamalizi udhia na kujiuzulu? Hapo tuu ndipo atakapofungua njia bora ya kusaka ufumbuzi kuambatana na katiba,wananchi watakapomchagua kansela mpya,mamoja ,mwanamke au mwanamme,uchaguzi mkuu wa bunge utakapoitishwa.Lakini mtoto wa ki-Niedersachse hataki kuingia katika daftari la historia kama mwanasiasa aliyeondoka kwa machungu.
Mada yetu ya pili inahusu hotuba ya rais George W. Bush wa Marekani kuhusu Irak.Gazeti maarufu la mjini Berlin „TAGESSPIEGEL linaandika:
„Mwaka mmoja uliopita wamarekani waliwakabidhi rasmi wananchi wa Irak ,hatamu za uongozi wa nchi yao.Na kwa vile bado hakuna usalama nchini Irak,sauti zinaziodi kupazwa nchini Marekani kutaka kujua lini wataihama nchi hiyo ya Ghuba.Rais George W. Bush hajakosea anapopinga madai kama hayo.Kwasababu ratiba ya kurejeshwa nyumbani wanajeshi wa Marekani itazidi kuwapa nguvu wanamgambo.Kuiacha Irak mikononi mwa magaidi,si jambo ambalo nchi za magharibi zitasubutu kulifanya.Kuondolewa wanajeshi wa Marekani hakutasaidia kuimarisha hali ambayo tokea hapo inatisha-kinyume chake ndicho kitakachoshuhudiwa.Waswahili wanasema mukiyavulia nguo ,yakoge.
Gazeti la mjinbi Cologne,Kölner Stadt Anzeiger linachambua:
„Kwamba rais George W. Bush anahutubia taifa kifua mbele,sababu ni moja tuu nayo ni hofu ya kuzuka wimbi la maandamano dhidi ya vita.Kwasasa bado wimbi kama hilo halijapiga nchini Marekani.Lakini cheche za chini kwa chini zimnaweza siku moja kuripuka.Vita visivyoleta tija haviwezi kuvumiliwa kwa muda mrefu.Yaliyotokea Vietnam yametufunza.“
Limeandika gazeti la Kölner Stadt Anzeiger.
Gazeti la THÜRINGER ALLGEMEINE la mjini Erfurt linaandika:
„Bush hana hila tena nchini Irak.Zaidi hamna katika hotuba yake.Kwanini lakini wananchi wenzake waendelee kuvumilia,rais Bush ameitaja sababu moja kubwa:Mashambulio ya kigaidi ya september 11.Sabaabu hiyo hiyo imetumiwa vya kutosha kuhalalisha vita dhidi ya Irak hata bila ya silaha za maangamizi kugunduliwa.Asili mia 58 ya walioulizwa maoni yao nchini Marekani wanahisi bado wanajeshi wao wasirejee.Wanahisi ,wakirejee itamaanisha wameshindwa.
Hoja kama hizo zimetolewa pia na gazeti la WIESBADENER KURIER.Gazeti linasema:
„Twende tuu! Hakuna jibu lolote jipya alilotoa rais Bush kukabiliana na hali inayozidi kutisha ya Irak.Hotuba ya rais George Bush imedhirisha jinsi sera zao kuelekea Irak zilivyo:hazina kichwa wala miguu.Kana kwamba hoja walizotoa kuteremka vitani hazijasutwa,anaendelea rais Bush kuitaja Irak kama uwanja muhimu wa mapambano dhidi ya ugaidi baada ya september 11.