Wahamiaji zaidi ya 500 nchini Ugiriki kuwekwa kizuizini
10 Julai 2025Hayo yametokea wakati Ugiriki inatekeleza hatua za dharura kwa ajili ya kushughulikia kuongezeka kwa wahamiaji wanoingia nchini humo kupitia kwenye Bahari ya Mediterania kutoka Libya. Wahamiaji hao watawekwa kizuizini.
Waziri Mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis, ametangaza kwamba nchi yake itasitisha kwa miezi mitatu zoezi la kuwaorodhesha wahamiaji wanaowasili kwa njia ya bahari kutoka Nchi za Afrika Kaskazini.
Hatua hiyo ya Ugiriki imechukuliwa wakati kuna mvutano wa kidiplomasia kati ya Umoja wa Ulaya na Libya kuhusu ushirikiano kwenye maswala ya uhamiaji. Maafisa wa Umoja wa Ulaya mapema wiki hii hawakuruhusiwa kuingia mashariki mwa Libya kusisitiza kutokukubaliana Libya na Umoja wa Ulaya juu ya muundo wa mazungumzo yaliyopangwa kuhusu kuzuia safari za wahamiaji.