Wahamiaji 7 wafariki dunia baada ya ajali ya boti Ugiriki
3 Aprili 2025Matangazo
Kituo cha Ugiriki cha ERT kimeripoti kuwa watoto wawili ni miongoni mwa waliofariki.
Polisi inasema watu 23 wameopolewa ila manusura wamesema watu 31 walikuwa wameabiri boti hiyo. Utafiti wa awali unaonyesha kuwa wahamiaji hao wametokea Afghanistan na Syria.
Watu wanaofanya biashara ya usafirishaji haramu hujaribu mara kwa mara kuwasafirisha wahamiaji Ulaya kutoka pwani za magharibi mwa Uturuki, Lebanon au Syria.
Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Wakimbizi UNHCR linasema angalau wahamiaji 125 walifariki dunia au walipotea mashariki ya Bahari ya Mediterenia mwaka 2024, ila walinzi wa pwani ya Ugiriki wanashuku idadi ya visa ambavyo havijaripotiwa viko juu zaidi.