Wahamiaji 68 wa Kiafrika wafa maji Yemen
4 Agosti 2025Matangazo
Kwa mujibu wa Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa (IOM), mashua hiyo iliyokuwa imebeba wahamiaji 154 kutokea Ethiopia ilizama kwenye Ghuba ya Aden, kusini mwa jimbi la Abyan, mapema hapo jana.
Mkuu wa IOM nchini Yemen, Abdusattor Eusov, ameliambia shirika la habari la AP kwamba miili 54 ilisombwa na maji hadi wilaya ya Khanjar, na mingine 14 ilipelekwa kwenye hospitali ya mji mkuu wa jimbo hilo, Zinjibar.
Ni watu 12 tu walionusurika kwenye ajali hiyo.
Hili tukio la karibuni kabisa miongoni mwa matukio kama hayo yanayopoteza maelfu ya roho wa wahamiaji wa Kiafrika wanaokimbia umasikini na vita kwenye nchi zao wakitarajia kuingia mataifa tajiri ya Ghuba.