SiasaUturuki
Wahalifu 234 wamekamatwa baada ya msako mkubwa barani Ulaya
15 Aprili 2025Matangazo
Waziri, Yerlikaya, amefahamisha kwamba wahalifu sugu 234 wa kundi moja la kihalifu wametiwa mbaroni, tisa kati yao walikuwa nje ya nchi na 225 walikuwamo ndani ya Uturuki. Waziri huyo wa mambo ya ndani wa Uturuki amesema msako wa wakati mmoja ulifanyika kwenye nchi za Uholanzi, Ujerumani, Uhispania, Ubelgiji na Uturuki. Maafisa walishirikiana kwa kupeana hati na taarifa za kijasusi. Katika msako huo tani 21.2 za mihadarati zilikamatwa. Waziri wa Uturuki Ali Yerlikaya, ameeleza kuwa magenge hayo ya kihalifu yalipanga kuingiza dawa ya kulevya nchini Uturuki na barani Ulaya kwa njia ya bahari kutoka Amerika ya Kusini, Afghanistan, Iran na kutoka kwenye nchi za Balkani.