Wagombea wanne wa Ukansela wapambana kwenye mdahalo
17 Februari 2025Matangazo
Kansela Olaf Scholz anayewania muhula wa pili ametetea rikodi ya serikali yake dhidi ya mashambulizi kutoka kwa wapinzani wake wakuu wa ambao ni Friedrich Merz wa muungano wa kihafidhina wa CDU/CSU na Alice Weidel wa chama cha mrengo mkali wa kulia cha AfD.
Soma pia:Merz akemea kauli za Makamu wa rais wa Marekani kuhusu Ulaya
Muungano wa Merz hivi sasa ndiyo unaongoza uchunguzi wa maoni ya wapiga kura ukiwa na asilimia 30 ikifuatiwa na asilimia 20 za chama cha AfD.
Mdahalo huo uliomjumuisha pia mgombea wa ukansela kutoka chama cha kijani, Die Grüne, Robert Habeck, umefanyika wiki moja kabla ya uchaguzi wa bunge mnamo Jumapili inayokuja.