Wagombea Urais Algeria wapewa kifungo cha miaka kumi jela
26 Mei 2025Mfanyabiashara wa kike Saida Neghza,waziri wa zamani Belkacem Sahli na jamaa yake kwa jina Abdelhakim Hamadi walihukumiwa kifungo cha miaka 10 jela, kwa makosa ya kutoa fedha ili kupata saini zilizokuwa zinahitajika kuingia katika kinyanganyiro cha kugombea urais mwezi Septemba.
Rais Tebboune ashida muhula wa pili Algeria
Tarehe 8 mwezi Mei, mwendesha mashitaka ya umma alipendekeza washitakiwa wapewe kifungo cha miaka 10 jela na faini ya dola 7,600 kila mmoja katika kesi iliyosikilizwa kwa siku tisa.
Watu wengine 70 wakiwemo watoto watatu wa Neghza, walipewa vifungo vya kati ya miaka mitano na nane jela.
Hakuna hata mmoja kati ya wagombea hao watatu waliofanikiwa kujisajili kugombea urais katika uchaguzi huo ambao rais wa sasa Abdelmadjid Tebboune alishinda kwa kishindo.