Wagombea urais wa zamani Algeria wafungwa jela
27 Mei 2025Matangazo
Mfanyabiashara Saida Neghza, waziri wa zamani Belkacem Sahli na Abdelhakim Hamadi ni miongoni mwa watu 70 waliohukumiwa kwenda jela hapo jana, ambapo wengine walifungwa baina ya miaka mitano na minane.
Watatu hao walikuwa wanataka kuwania urais kwenye uchaguzi wa Septemba, lakini wote walizuiwa na mamlaka za uchaguzi na badala yake kushitakiwa kwa kujaribu kununuwa saini za watu wa kuwaunga mkono.
Miongoni mwa walioshitakiwa walikuwa watoto watatu wa kiume wa mfanyabiashara Saida Neghza.
Wote wanakanusha kuhusika na ufisadi wowote na badala yake wanaelezea hukumu dhidi yao kuwa ni adhabu ya kumkosowa Rais Abdelmajid Tebboune kwa uongozi wake mbaya.