Wafuasi wa Navalny wazuru kaburi lake mjini Moscow
16 Februari 2025Raia wa Urusi takriban 1,500 ambao ni wafuasi wa kiongozi wa upinzani nchini humo hayati Alexei Navalny walikusanyika katika kaburi lake leo mwaka mmoja baada ya Navalny kuaga dunia. Wafuasi hao walionekana wakiweka mashada ya maua katika kaburi hilo.
Navalny mpinzani wa rais wa Urusi Vladimir Putin aliyetangazwa kuwa mtu aliye na misimamo mikali, alifariki tarehe 16 februari mwaka jana katika jela alikokuwa akizuiliwa nchini humo.
Kasisi aliyeongoza ibada ya mazishi ya Navalny aadhibiwa na kanisa Orthodox Moscow
Mataifa ya Magharibi yanaamini Navalny aliuwawa na serikali ya Urusi japo utawala wa nchi hiyo haujazungumzia kwa uwazi juu ya kifo chake. Mama yake Navalny Lyudmila Navalnaya amewaambia waandishi habari kwamba anafanya kila awezalo kuhakikisha uchunguzi unafanyika kubaini kifo cha mwanawe lakini pia anatumai waliohusika watawajibishwa.