WAFARANSA 3 WAULIWA IRAQ:
7 Januari 2004Matangazo
BAGHDAD: Wananchi 2 wa Kifaransa wamefariki na 1 amejeruhiwa baada ya kupigwa risasi nchini Iraq.Watu hao 3 walikuwa watumishi wa kampuni ya Kimarekani inayohusika na kazi za ujenzi wa Iraq karibu na mji wa Fallujah.Kwa upande mwingine katika mji wa Basra kusini mwa Iraq,polisi wa Kiiraqi waliwafyetulia risasi wanajeshi wa zamani wa Kiiraqi waliokuwa wakiandamana kudai mishahara yao ya miezi ya nyuma.Mtu mmoja aliuawa na wengine watatu walijeruhiwa.Wafanya maandamano hao walijaribu kuingia kwa nguvu katika tawi la ofisi ya Benki Kuu.Wanajeshi wa Kingereza baadae waliingilia mapambano hayo kurejesha hali ya utulivu.