SiasaMarekani
Wafanyakazi wa USAID wasimamishwa kazi kwa muda
5 Februari 2025Matangazo
USAID imeeleza kuwa wafanyakazi wake walioko nje watarudishwa nyumbani, ingawa pia limesema hatua hiyo haitowagusa wafanyakazi wenye majukumu maalum.
Soma pia: Athari za ukataji misaada wa Marekani kwa Uganda
Uamuzi huo ni sehemu ya ya mageuzi ya serikali ya Marekani inayoongozwa na Donald Trump na bilionea Elon Musk ya kutaka kupunguza matumizi na imesababisha hasira na upinzani mkubwa kutoka chama cha Democratic na jumuiya ya mashirika ya haki za binadamu.
USAID ni shirika la msaada la Marekani linalofadhili miradi kiafya na masuala ya dharura katika mataifa 120 duniani ikiwemo mataifa masikini kabisa ya ulimwengu.