Wafanyakazi kadhaa nchini Ujerumani wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha huku wakishindwa kumudu kodi za nyumba licha ya kuwa na ajira. Nyumba za kupanga ni vigumu kuzipata na bei yake ni kubwa, hasa kwenye miji kama Berlin na hivyo sio rahisi kwa watu wenye vipato vya chini kumudu kodi za mijini. Mtayarishaji wa Makala ya Sura ya Ujerumani ni Zainab Aziz.