SiasaAsia
Wafanyakazi nchini India wafanya mgomo wa kitaifa
9 Julai 2025Matangazo
Wito wa mgomo huo, uliopewa jina la Bharat Bandh (ikimaanisha "Funga India"), umetolewa na muungano wa vyama 10 vikuu vya wafanyakazi, vinavyowakilisha makundi ya vibarua, wakulima na wafanyakazi wa vijijini.
Shughuli mbali mbali zasitishwa
Kwa mujibu wa muungano huo, shughuli za uchimbaji wa makaa ya mawe zimesimama katika majimbo kadhaa, huku baadhi ya safari za treni zikisitishwa baada ya waandamanaji kufunga njia za reli.
Aidha, shughuli katika benki, makampuni ya bima na maduka makubwa pia ziliripotiwa kutatizwa.
Migomo hii inazidi kuwa changamoto kwa juhudi za Modi kuvutia wawekezaji wa kigeni, kupitia sera za kulegeza sheria za kazi, kuimarisha mazingira ya biashara, na kuongeza uzalishaji nchini humo.