Wafanyakazi 5 wa mashirika ya misaada wauawa Sudan
4 Juni 2025Matangazo
Katika taarifa ya pamoja, mashirika ya Umoja wa Mataifa yamesema kuwa msafara wa malori 15 uliopangwa na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, na lile la watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF, ulishambuliwa siku ya Jumatatu karibu na kijiji cha Al-Koma katika jimbo la Darfur Kaskazini.
Umoja wa Mataifa waelezea wasiwasi wake juu ya ongezeko la wakimbizi wa Sudan wanaoingia Chad
Taarifa hiyo imeongeza kuwa watu watano wameuawa na wengine kadhaa kuachwa na majeraha huku malori kadhaa yakiteketezwa na bidhaa muhimu za kibinadamu kuharibiwa.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ametoa wito wa uchunguzi kufanywa kuhusiana na shambulizi hilo la hivi karibuni zaidi.