UchumiAfrika
Wafadhili waahidi dola bilioni 8 kusambaza umeme Afrika
29 Januari 2025Matangazo
Mpango huo unaoitwa "Mission 300" uliozinduliwa na Benki ya Dunia na Benki ya Maendeleo ya Afrika mwezi Aprili, unakadiriwa kugharimu dola bilioni 90.
Utekelezwaji wake hata hivyo unakabiliwa na changamoto kutokana na uchumi dhaifu wa mataifa ya Afrika, hasa kutokana na makusanyo duni ya mapato na gharama kubwa za mikopo.
Viongozi kwenye Mkutano wa kilele wa Nishati barani Afrika uliofanyika Dar es Salaam, Tanzania wamesema nusu ya walengwa hao wataunganishiwa umeme wa gridi za taifa zilizopo, na nusu nyingine itatokana na vyanzo vya nishati mbadala, ikijumuisha gridi ndogo za upepo na jua.