Wadukuzi waiongezea Pyongyang sarafu za kidigitali
7 Aprili 2025Wataalamu wameiambia DW kwamba, kwa miaka ya hivi karibuni wadukuzi wa Korea Kaskazini wameiba sawa na mabilioni ya dola na taifa hilo linatafuta kukusanya utajiri zaidi kupitia njia zisizo halali.
Wadukuzi kutoka genge la Lazarus--genge mashuhuri la wizi wa sarafu za mtandaoni Korea Kaksazini liliiba kiasi cha dola bilioni 1.5, sarafu za mtandaoni kutoka kampuni ya kubadilisha sarafu hizo ya nchini Dubai ya ByBit, mnamo mwezi Februari.
Kampuni hiyo imesema kwamba wadukuzi hao walifanikiwa kuipata hazina yake ya kidigitali ya Ethereum, ambayo ni ya pili kwa ukubwa baada ya ile ya Bitcoin.
Soma pia:Mahakama yaruhusu udukuzi wa simu Munich
Binance News, jukwaa jipya linaloendeshwa na kampuni ya ubadilishaji wa fedha za kidijitali Binance, liliripoti mwezi uliopita kwamba Korea Kaskazini sasa ina takriban Bitcoin 13,562, sawa na dola bilioni 1.14.
Bitcoin ni sarafu ya kidijitali kongwe na inayojulikana zaidi duniani, mara nyingi ikilinganishwa na dhahabu kutokana na kustahimili mfumuko wa bei.
Pyongyang imefanikiwa kupitia wizi mtandaoni
Kwa mujibu wa Binace kwa sasa ni Marekani na Uingereza pekee zinazoshikilia akiba kubwa zaidi ya sarafu hiyo.
"Tusizungumze kwa mafumbo — Korea Kaskazini imefikia hapa kupitia wizi,” Aditya Das, mchambuzi katika kampuni ya utafiti wasarafu za kidijitali Brave New Coin, New Zealand, aliiambia DW.
"Mashirika ya kimataifa ya polisi kama FBI yameonya hadharani kwamba wadukuzi wanaofadhiliwa na serikali ya Korea Kaskazini wanahusika na mashambulizi kadhaa kwenye majukwaa ya fedha za kidijitali,” aliongeza.
Mchambuzi huyo mesisitiza kwamba licha ya indhari hiyo,bado kampuni za fedha za kidijitali zinaibiwa na wadukuzi wa Korea Kaskazini wanazidi kuwa na mbinu za kisasa katika kutekeleza uhalifu.
Soma pia:Wadukuzi wa China wazilenga simu za wagombea urais nchini Marekani
Wadukuzi waliobobea wa Korea Kaskazini huwa wanatumia muda kabla ya ya kujipenyeza kwenye shirika halali la kimataifa, na mara nyingi hujifanya wawekezaji kwenye mitaji, waajiri au wafanyakazi wa TEHAMA ili kujenga uaminifu na kuepuka mifumo ya ulinzi kwenye makampuni.
Mara fedha za kidijitali zinapoibiwa, Das anasema urejeshaji ni "nadra sana.” kutokana na mifumo ya fedha za kidijitali kubuniwa kufanya miamala isiyoweza kubatilishwa na kupambana na wadukuzi wa Korea Kaskazini.
Wachambuzi: Utawala wa Kim Jong Un 'unasaidiwa' na wizi wa mitandaoni
Profesa wa sheria katika Chuo Kikuu cha Dankook Park Jung-won, anasema hapo awali Korea Kaskazini ilitegemea miamala hatari kama vile kusafirisha mihadarati na bidhaa bandia au kutoa wakufunzi wa kijeshi kwa mataifa ya Afrika - ili kujipatia fedha haramu.
Mtaalamu huyo wa sheria ameongeza kwamba ujio wa sarafu za kimtandao umekuwa ni fursa kubwa kwa Korea kaskazini.
"Fedha wanazoiba zinaenda moja kwa moja kwa serikali na zinatumika kwa silaha na teknolojia kubwa ya kijeshi pamoja na familia ya Kim," Park aliiambia DW.
Soma pia:Akaunti ya Twitter ya Obama, Biden zadukuliwa
Park haamini kwamba shinikizo la nje lingeliweza kulazimisha Korea Kaskazini kusitisha mashambulizi yake ya udukuzi wa mtandaoni.
"Wamezoea chanzo hiki cha mapato, hata kama ni haramu, na hawatabadilika,” aliongeza kwamba kwa sasa hakuna sababu ya makusudi kwao kuanza kufuata sheria za kimataifa na hakuna njia ya kuongeza shinikizo.
Das anakubali kwamba kiutendaji kuna baadhi ya makampuni hayatoi kipaumbele kwenye suala zima la usalama, jambo ambalo linaweza kuhatarisha usalama wa kampuni.